Tanzanite Vs Diamond

Harufu ya bifu zito kati ya wasanii chipukizi wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Mwingereza Athuman Mwingereza ‘Tanzanite’ na Nassib Abdul ‘Diamond’ sasa imefika puani kufuatia kukutana ‘laivu’ kwa wawili hao.

Diamond anatamba kitaani na kibao chake cha ‘Mbagala’ huku Tanzanite akidaiwa ‘kuuiga’ wimbo huo kwa sauti na ‘biti’ katika wimbo wake wa ‘Kafara’.

Katika kipindi cha ‘Saturday Night Live’ kilichorushwa angani na runinga ya Channel Five (EATV) Ijumaa iliyopita, wasanii hao walikutana ‘laivu’ na kidogo ‘pasitoshe’ baada ya Diamond kuonyesha wazi hasira zake dhidi ya Tanzanite.

Mzuka ulipanda zaidi kufuatia ‘Prizenta’ wa kipindi hicho, Jimmy Kabwe kumuuliza Tanzanite ni kwanini alikopi wimbo huo kwa sauti na biti, ambapo alijibu alikuwa akijaribu lakini akashangaa kusikia wimbo huo unarushwa hewani na vituo vya redio Bongo.

Katika majibu yake, Diamond alisema msanii huyo ni muongo ‘mkubwa’ na kwamba, tayari yeye ameshampeleka msanii huyo kwenye ‘mahakama’ ya COSOTA licha ya kwamba, hajui ni kwanini mpaka sasa chama hicho cha kusimamia kazi za wasanii hakijamchukulia hatua Tanzanite.

Tutegee sikio hili litaendeleaje!…

Angalia ‘Mbagala’ ya Diamond

{youtube}hZBXVkAcbWo{/youtube}

Angalia ‘Kafara’ ya Tanzanite

{youtube}H0rvEC1ApDU{/youtube}

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW