Michezo

TANZIA: Ajiua baada ya kuhusishwa katika kashfa ya rushwa na FIFA

Afisa wa zamani wa soka nchini Argentina amejiua baada ya kuhusishwa katika kashfa ya rushwa iliyotajwa mjini New York.

Jorge Delhon amejirusha kwenye reli na kukanyagwa na treni kwenye mji mkuu wa Argentina Buenos Aires.

Baadhi ya viongozi wa soka nchini Argentina wameelezea kusikitishwa na tukio hilo na kusema limetia doa kwenye soka la nchi yao.

Kesi ya Delhon iliyofunguliwa siku ya Jumatatu inafuatia upelelezi wa muda mrefu uliofanywa na Marekani kwenye shirikisho la soka duniani FIFA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents