Burudani ya Michezo Live

TANZIA: Beki wa Azam fc Agrey Moris afiwa na mke wake wakati anajifungua, Klabu yake yatoa ujumbe huu

TANZIA: Beki wa Azam fc Agrey Moris afiwa na mke wake wakati anajifungua, Klabu yake yatoa ujumbe huu

Nahodha wa Azam FC, Agrey Morris amefiwa na mkewe usiku wa leo jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kumalizika mchezo wa nusu fainali ya Mapinduzi Cup dhidi ya Simba. Agrey hakuwepo kwenye kikosi cha Azam kilichoenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya kumuuguz Sidebar a mkewe ambaye alikuwa mjamzito.


……
Ujumbe wa klabu ya @azamfcofficial “Azam FC tumepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mke wa Nahodha wetu, Agrey Moris, aliyefariki dunia jana jioni wakati akiwa kwenye harakati za kujifungua. Tunatoa salamu zetu za pole kwenda kwa familia ya Moris, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huo.

Azam FC tunaungana na familia ya marehemu na tunamuomba Mwenyezi Mungu, awajalie nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Bwana ametoa na Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen. #RIPMpendwaWetu

Chanzo Azam Fc.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW