Shinda na SIM Account

TANZIA: Mamia ya watu wafariki dunia Mexico

Nchi ya Mexico imekumbwa na janga kubwa la tetemeko la ardhi ambalo limesababisha vifo vya watu zaidi ya 140 Jumanne hii.

Tetemeko hilo linalodaiwa kuwa na ukubwa wa 7.1 limeanguja nyumba zaidi ya 30 katika mji wa Mexico City na watoto 30 hawajulikani walipo.

Baada ya kutokea janga hilo, rais wa nchi hiyo Enrique Peña Nieto amesema kuwa wanakabiliwa na dharura ya taifa lao. Hata hivyo rais wa Marekani, Donald Trump ametuma salamu zake za pole kwa nchi hiyo kupitia mtandao wa Twitter kwa kuandika, “God bless the people of Mexico City. We are with you and will be there for you.”

Wakati huo huo tetemeko hilo limesababisha madhara katika majimbo ya mengine ya karibu kama Morelos na Puebla.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW