Habari

TANZIA: Meya wa zamani wa Dar es Salaam amefariki dunia

Aliyekuwa Meya  katika jiji la Dar es Salaam  mwaka 2000-2005,  Kleist Skyes  amefariki dunia  leo Novemba 22, mwaka huu wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan.

Mwanamuziki wa kizazi kipya, Dully Sykes ambaye Kleist ni baba yake mkubwa akizungumza na Mwananchi amesema meya huyo wa zamani amefariki dunia leo saa mbili asubuhi.

“ Yaah, kweli amefariki na sasa familia tumeanza kukutana kujua mazishi yatafanyika lini,” amesema.

Meya wa sasa wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza na Mwananchi amesema hivi karibuni alimtembelea hospitalini alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na tatizo la moyo.

Mwita amesema kuna wakati Sykes alimtembelea ofisini kwake na alimpa ushauri kuhusu utendaji kazi.

“Ni mtu tuliyeelewana, amewahi kuja hapa ofisini kwangu kama mara mbili na kunishauri haya na yale kuhusu kazi zangu,” amesema.

Kleist Sykes aliyekuwa diwani wa Kivukoni mwaka 2000 hadi 2005 anatoka katika familia ambayo ni miongoni mwa zenye wanasiasa walioshiriki katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Chanzo na Mwananchi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents