Tupo Nawe

TANZIA: Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraem Kibonde amefariki dunia

Mtangazaji wa Clouds Fm, Ephraem Kibonde amefariki dunia leo alfajiri mkoani Mwanza.

Taarifa za awali zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella zinadai kuwa Kibonde alipandwa na presha kwenye msiba wa Ruge Mutahaba mkoani Bukoba, jambo lilimfanya asafirishwe kwenda Mwanza kwa matibabu.

Katika kuthibitisha hilo Clouds Fm wametoa taarifa rasmi iliyosomeka “Tukiwa bado na majeraha mabichi ya msiba wa Mkurugenzi wetu wa Vipindi na Uzalishaji #RugeMutahaba, kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha Mtangazaji wetu #EphraimKibonde kilichotokea alfajiri ya leo (Machi 7 2019)

Tunamtukuza Mungu kwa Maisha ya Kibonde, na kumuomba yeye ampokee na kumpuzisha katika makao ya amani ya milele.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW