HabariUncategorized

TANZIA: Muigizaji nguli wa filamu nchini India, Shashi Kapoor aaga dunia (+Video)

Muigizaji mkongwe wa filamu nchini India, Shashi Kapoor amefariki dunia leo katika Hospitali ya Kokilaben mjini Mumbai akiwa na umri wa miaka 79 .

Shashi Kapoor

Bw. Kapoor, alitamba na filamu maarufu kutoka Bollywood kama vile Trishul (1978), Namak Halaal(1982), Deewar (1995), Kabhie Kabhie (1976) na nyingine nyingi, amekuwa akiugua kwa muda kabla ya kukutwa na mauti siku ya jana.

Shashi anatoka katika familia ya vipaji ya Kapoor ambayo imetawala tasnia ya filamu za Kihindi kwa miongo mingi.

Katika enzi za uhai wake Kapoor alishawahi kushinda tuzo nyingi za filamu za taifa na alitunukiwa tuzo kuu ya heshima ya  Padman Bhushan inayotolewa na raia wa India mwaka 2011.

Mbali na filamu za kihindi Kapoor ameigiza pia na wasanii wengine kutoka Marekani, Uingereza na Urusi kama filamu ya Vozvrashcheniye Bagdadskogo Vora ya mwaka 1988.

Kwa mujibu wa mtandao wa Hindu Times, Kapoor amefariki kwa ugonjwa wa figo ambao ulikuwa unamsumbua kwa miaka mingi.

Tayari Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ametoa pole kwa familia ya marehemu Kapoor kwa kutumia ukurasa wake wa Twitter.

Jikumbushe hapa baadhi ya filamu zake alizowahi kuigiza enzi za uhai wake

https://youtu.be/7n4n-pEwD1A

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents