TANZIA: Mwili wa Yassin Abdallah (Ustaadh) kuzikwa saa 7

Aliyewai kuwa Rais wa ngumi za kulipwa Yassin Abdallah Mwaipaya (Ustaadh) anatarajiwa kuzikwa leo Buza Kanisani majira ya saa 7:00 mchana.

Hayo yameelezwa na mdogo wa marehemu, Salehe Abdala Mwaipaya ”Mazishi yatakuwa leo saa 7:00 mchana Buza Kanisani maarufu kama makaburi ya City. Taratibu za mazishi bado zinaendelea.”

SuperD Boxing Coach: YASSIN ABDALLAH ASHUKURU KAMATI YA UTENDAJI YA E&CAPBA

Yassin Abdallah (Ustaadh) ambaye alikuwa rais wa ngumi za kulipwa TPBO, alifariki hapo jana asubuhi siku ya Jumanne ya Septemba 7/2020.

Kwa upande wake Emmanuel Mlundwa ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu ameeleza Namshukuru Mungu kunipa muda wa kukaa naye sana, kabla ya kufariki alinipigia simu nikiwa Mpanda na kuniomba nije kumsaidia kulisimamia pambano lake la WBF lilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City. Taarifa yake nimeshtuka sana na kuhuzunika ila kazi ya Mungu haina makosa.”

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW