Burudani

TaSuBa kuzindua mafunzo ya sanaa kwa Vijana

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kushirikiana na Tulia Trust wanatarajia kuzindua rasmi mafunzo maalumu ya sanaa kwa vijana 27 kutoka Mkoani Mbeya.

Tukio ambalo linatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi (kesho) ya Aprili 29.2017, katika wilaya ya Bagamoyo ambapo, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb.) anatarajia kuwa mgeni rasmi.

Mafunzo haya ya sanaa yamegawanyika katika awamu mbili; kwa awamu ya kwanza, ina jumla ya vijana 20 ambao tayari wameshaanza mafunzo chuoni ambayo yatadumu kwa muda wa miezi miwili ,yakihusisha kujifunza uchezaji ngoma za asili ya Tanzania, ngoma za ubunifu, muziki wa asili ya Tanzania, uigizaji, matumizi ya jukwaa na maleba.

Kwa awamu ya pili, vijana 7 watapata mafunzo katika ngazi ya stashahada (diploma) na Astashahada (certificate) katika fani za sanaa za maonyesho na ufundi (performing and visual arts).

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents