TASWA yapongeza wanawake wa gofu
CHAMA cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) kimetoa pungezi kwa kwa timu ya gofu ya Taifa ya wanawake ambayo mwisho mwa wiki ilitoa kimasomaso na kuweka historia katika michuano ya gofu ya wanawake kombe la Challenge Afrika baada ya kufanya vizuri na kushika nafasi ya pili kwenye michuano hiyo iliyofanyikia katika viwanja vya Klabu ya IBB International mjini Abuja.
Amiri Mhando,Katibu mkuu wa TASWA alisema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema, Tanzania ilishika nafasi ya pili kati ya nchii 4 baaada ya kukusanya mikwaju ya 472 katika ya raundi ya tatu za viwanja vya IBB vyenye par 74 huka Afrika ya Kusini ilitetea taji hilo na kuibuka bingwa katika mchezo huo kwa kupata mikwaju 440 huku Zimbabwe ijinyakulia nafasi ya tatu kwa kupata mikwaji 475 na ikifwatiwa na Zambia iliyopata mikwaju 485.
Tunaseama tunawapongeza timu ya wanawake na wadau wengine wote waliowawezesha kwani ni mara ya kwanza timu ya gofu ya wanawake kufanya vizuri , hasa tukikumbuka michuano iliyofanyika Cairo mwaka 2008 Tanzania ilishika nafasi ya 8.
‘Taswa tumefurahishwa sana na pia tunawaomba wachezaji wa gofu waliotoka Abuja ambao ni Hawa Wanyeche Madina, Iddi na pamoja na Shazi Myombe, wasibwete na kujisahau bali waongeze juhudi na kuzidi kuitangaza nchi,’ alisema Mhando.