Tupo Nawe

Tathimini ya uchaguzi wa serikali za mitaa watolea na mashirika haya “Uchaguzi ulikuwa wa huru” – Video

Tathimini ya uchaguzi wa serikali za mitaa watolea na mashirika haya "Uchaguzi ulikuwa wa huru" - Video

Mashirika yasio ya kiserikali Action for Change (ACHA) na The Right Way (TRW) yaliyoungana ili kutoa elimu ya uraia, elimu ya mpiga kura na uangalizi wa uchaguzi baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Alisema malengo mengine ni pamoja na kutoa Elimu ya uraia na mpiga kura, kuangalia uchaguzi hususani mwenendo na maandalizi kabla ya mchakato wa uchaguzi, uandikishaji, kampeni, upigaji kura, kuhesabu kura na hatimaye kutangaza matokeo.

“Utazamaji katika uchaguzi huwa na malengo makuu mawili ambayo ni pamoja na   kujenga kujiamini kwa makundi mbalimbali ya uchaguzi wakiwemo wapiga kura na wananchi kwa ujumla na kupelekea kuamini matokeo yanayotangazwa.

Pia kupata mafundisho yatokanayo na mchakato mzima wa uchaguzi, jambo ambalo husaidia kufanya masahihisho katika michakato ijayo hususan kwenye Katiba, Sheria au Kanuni za utendaji wake.

Alisema kasi ya uandikishaji wa Wapiga Kura ilishuka kuanzia tarehe 8 – 14 Novemba, 2019. Hata hivyo baada ya kuongezwa siku tatu (3) za ziada za kujiandikisha kasi ilianza kuongezeka. Taarifa ya kutoka kwa watazamaji wa TanEA na vyombo vya habari zinaonyesha kuwa zoezi hilo lilikwenda vizuri licha ya kujitokeza changamoto ndogo ndogo ikiwemo mwamko mdogo wa watu kujiandikisha hali iliyo lazimu kuongezwa muda.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW