Habari

Tatiana asherekea Bongo

Mwakilishi wa Angola katika Shindano la pili la Big Brother Africa Tatiana Jana usiku alisherehekea siku yake ya kuzaliwa katika party iliyofanyika katika ukumbi wa Stallion Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Sherehe hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu kiasi wakiwemo waandishsi wa habari, walimbwende, wafanyakazi wa makampuni mbalimbali na wapenda bata za kiaina ilianza kwa kusuasua mida ya saa 3 na nusu usiku na kushika kasi mida ya saa sita ya usiku baada ya Tatiana na nduguze kuwasili.

Dj wa sherehe hiyo Dj elly toka Angola alifanya mavitu ya ukweli ambapo alidondosha pini kali kutoka kwa wasanii wa Angola,africa Mashariki na sehemu zinginezo duniani na kuwafanya wahudhuriaji kupagawa.

Akiongea wakati wa kutoa nasaa kabla ya kukata keki na kufungua shampeni Tatiana ambaye kwa muda mwingi usiku huo alikuwa na furaha alisema anawashukuru watanzania kwa sapoti waliyompa tangu alipotoka kwenye jumba la Big Brother 11. akiendelea alisema aliamua kufanya Birthday Pati kwenye ardhi ya Tanzania na sio kwao Angola kwa sababu alijiona anahitaji kufanya kitu spesho kwa watanzania kama shukrani ya upendo wao kwake.

Aidha Tatiana aliwashangaza waliohudhuria sherehe hiyo kwa kumwalika mama yake kutoa nasaha chache ambapo na yeye hakumwangusha mwanae zamu yake ilipofika. Aliimba nyimbo ya Malaika ambayo ilitamba Africa mashariki kwa kipindi kirefu kuanzia miaka ya themanini na kuamsha mayowe toka kwa wahudhuriaji.

Sherehe hiyo ilipata udhamini wa kinywaji cha Savannah Cider.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents