Tatiana wa Big Brother Kushuka nchini

Yule mshindi wa wa pili wa shindano la Big Brother Afrika 2,Tatiana Durao wa Angola anatarajia kushuka nchini Aprili 22 katika ziara fupi itakayoambatana na maonesho mbalimbali ya mavazi na urembo

Tatiana


 


Yule mshindi wa wa pili wa shindano la Big Brother Afrika 2,Tatiana Durao wa Angola anatarajia kushuka nchini Aprili 22 katika ziara fupi itakayoambatana na maonesho mbalimbali ya mavazi na urembo.


 


Mratibu wa ziara hiyo, Peter Mwendapole, alisema ujio wa Tatiana unatokana na kuonesha mchango mkubwa wa kuitanagaza Tanzania katika ziara zake za nchi za jirani kwa kuvaa kilemba cha bendera ya Tanzania hivyo hakuna sababu ya kutomualika nchini kwetu.


 


Aidha Tatiana alikuwa kivutio na mchango mkubwa katika ushindi wa mwakilishi wa Tanzania katika mashindano hayo mwaka jana Richard, ambapo akiwa ndani ya jumba hilo alikuwa akivaa kitambaa cha bendera ya Tanzania, huku akoinesha kuwa na mapenzi na nchi yetu dhidi ya kijana Richard.


 


Alisema ujio huo pia utakuwa kwa ajili ya onesho la mavazi litakaofanyika Aprili 26 na watashiriki warembo mbalimbali nchini.
Magazeti mengi ya udaku nchini yamekuwa yakiuhusisha ujio wa binti huyo na mapenzi yalee ambayo alikuwa nayo dhidi ya Richard, lakini yetu sisi macho tu.


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents