Tattoo mpya ya Neymar yawachanganya mashabiki

Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA) katika hatua ya 16 bora inatarajiwa kuanza kutimua vumbi usiku wa leo (Jumanne) kwa mechi mbili kuchezeka – mshambuliaji wa klabu ya soka ya PSG, Neymar amewaacha mashabiki midomo wazi.

Wakati Real Madrid kesho ikitarajiwa kuwakaribisha PSG katika uwanja wake wa Santiago Bernabéu kwenye hatua hiyo, Neymar amechora tattoo mpya ya mchoro wa kombe la michuano hiyo kitendo ambacho kimetafsiriwa na baadhi ya mashabiki kuwa anauhakika kulibeba kombe hilo kwa mwaka huu.

Neymar alisajiliwa na PSG mwanzoni mwa simu huu akitokea Barcelona kwa kitita cha paundi milioni 198 ambapo ndio mchezaji anashikilia rekodi ya mchezaji aliyesajiliwa kwa fedh nyingi zaidi duniani.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW