Burudani

Tatueni matatizo yenu ya uhusiano ndani kwanza – Mwasiti

Mwasiti Almasi ametoa somo muhimu kuhusu mahusiano kwa mashabiki wake nchini.

Mwasiti

Muimbaji huyo ameiambia E-News ya EATV kuwa watu wanatakiwa kutatua matatizo yao ya mapenzi au mahusiano pasipo kuwashirikisha watu.

“Mapenzi ni kitu kingine kabisa, kila mtu atasema la kwake kwa namna yake na kitu kibaya zaidi tumeumbwa kuvumilia ama kutokuvumilia pia. Wakati mwingine utausemea moyo kwa kujiamini huku ukiamini umeshinda, wakati mwingine utavuka mipaka kwa kunyooshea mapenzi ya wengine vidole kwa vicheko vya kebehi ukihisi yako ndio yako sawa,” amesema Mwasiti.

“Unalalamika kila siku kuhusu mtu wako (mpenzi) kuwa ana matatizo na mara zote mnayapeleka kwa watu kusuluhisha. Hebu sema naye kaeni chini myamalize mambo yenu maana wengine wanawacheka wanafurahi kuona mizengwe yenu kila mara, utajuta, utalia na kadhalika lakini ujue msuluhishi wa kwanza ni wewe kwanza. Kwahiyo basi sema naye mtu wako kwa namna yoyote ile uweke hayo mahusiano yako pahala salama. Ukiyapeleka kwa marafiki, washkaji, basi ujue hiyo ni stage ya mwisho labda.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents