Michezo

Taylor amchakaza MacCaskill pambano la WBA

Mwanamasumbwi, Katie Taylors ameudhihirishia ulimwengu kuwa yupo fiti katika mchezo huo baada ya hapo jana usiku siku ya Jumatano kumpiga mpinzani Jessica McCaskill na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa wadunia wa WBA uzito wa lightweight kwa mara ya kwanza pambano lililopigwa huko York Hall.

Mwanamasumbwi, Katie Taylors (Kulia) akipigana na Jessica McCaskill (kushoto)

Mara baada ya ushindi huo uliyomuwezesha kutwaa mkanda wa dunia wa WBA kwa mara ya kwanza, Taylor amesema kuwa ulikuwa mchezo mgumu mno tangu kuanza kucheza masumbwi ya kulipwa.

Mwanamasumbwi, Katie Taylors akitangazwa Bingwa wa WBA

“Ulikuwa mchezo mgumu kwangu toka kuanza kucheza masumbwi ya kulipwa. Nilijua kuwa nilipaswa kujituma kwa uwezo wangu wote ili kushinda hasa ukizingatia napigana hapa York Hall mahali ambapo hutamani kupigania kila pambano langu,”amesema bondia huyo mwanadada Taylor.

Mwanamasumbwi, Katie Taylors

Katie Taylors ameongeza “Nimezaliwa kufanya hivi, naishi ndoto za maisha yangu. Hatakama kuna mikanda mingine nitahitaji yote hiyo niitwae kwa sababu nahitaji kuweka historia katika mchezo huu.”

Dunia kushuhudia pambano kali Taylor Vs MacCaskill

Taylors mwenye umri wa miaka 31, amepigana jumla ya mapambano nane huku akishinda yote bila kupoteza hata moja ilihali matano yakiwa kwa KO.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents