Michezo

Tazama Anthony Joshua Vs Joseph Parker walivyotambiana baada ya kupima uzito

Mara baada ya zoezi hilo la vipimo kukamilika wawili hao Anthony Joshua na Joseph Parker kila mmoja amepata kuzungumza na vyombo vya habari na ndipo tambo zikaanza.

Wakati mabondia hao walipokutana hii leo kwenye zoezi la kupima uzito Cardiff

Picha: Anthony Joshua na Joseph Parker wakutana uso kwa uso kabla ya pambano lao Jumamosi hii

Najiskia vema, mazoezi yangu yamekwenda vizuri nadhani umeona mwenyewe nimepungua hadi kilo.  Kupungua kwangu uzito kutaniongezea kuwa mwepesi na haraka zaidi kuliko hata mwanzo.

Mpinzani wangu namuona yupo vizuri na nibingwa wa dunia ila nitafanya vizuri usiku wa kesho mwenye utashuhudia na nimejiskia furaha kuonana nae uso kwa uso kama hivi.  Mimi ni bingwa wa dunia kwa hiyoa akilini mwangu najua naenda kukutana na bingwa mwenzangu wa WBO.

 Parker yupo fiti kumvaa Anthony Joshua wiki hii – Scott

Kwa upande wa Joseph Parker amesema kuwa yupo tayari kwa pambano hilo linalotarajiwa kupigwa hapo kesho siku ya Jumamosi.

Kabla ya pambano dhidi ya Anthony Joshua bondia Joseph Parker amtafuna samaki mbichi

Mpaka hapa tulipofikia kilakitu kimekamilika wachanifikirie kuhusu pambano hili kwa kuwa najua atakuwa yupo makini.

Tunafanana, sote tutakuwa na malengo sawa ulingoni hapo kesho nimemuona ni mtu mwenye kujiamini ninaamini ni mpambanaji mzuri.

Parker ameongeza Raundi za mwanzo chochote kinaweza kutokea itategemea kila mmoja ameingia na mpango upi mzuri zaidi ya mwenzake, nipo tayari kwa chochote. Nipo hapa kwa vita  utalazimika kufanya kilakitu ili uweze kunipiga.

AJ mwenye umri wa miaka 28 ataingia uwanja wa Principality uliyopo Cardiff huku akiwa na rekodi ya kutopoteza pambano hata moja kati ya 20 yote aliyocheza na kumkabili mpanzani wake Parker ambaye na haja poteza hata moja kati ya 24 aliyopigana.

Wawili hao wataingia uwanjani hapo kesho siku ya Jumamosi ya tarehe 31 ya mwezi Machi kila mmoja kutaka kutengeneza historia yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents