Burudani

Tazama kwa picha jinsi Akon anavyowaabisha wanasiasa wa Afrika kwa mradi wake wa kusambaza umeme kwa waafrika milioni 600

Akon amepania kubadilisha maisha ya waafrika milioni 600 kwa kuwasambazia umeme wa jua.

Kufanikisha hilo, Akon ataanzisha chuo maalum cha kufundisha elimu ya umeme wa jua kwa wanafunzi ambao watasaidia kusambaza umeme huo kwenye makazi ya waafrika maskini.

akon 2
Mafundi wa mradi wa Akon wakiendelea na kazi ya kufunga taa za barabarani zinazotumia umeme wa jua

Akon, anayetokea nchini Senegal na aliyekua bila umeme, ameuita mradi huo kwa jina la ‘Akon Lighting Africa.’ Mradi huo pia utazalisha ajira kwa vijana.

akon 3

Mwanafunzi kwenye chuo hicho cha Akon atajifunza mchakato wote wa kufunga na kutumia vifaa vinavyozalisha umeme wa jua. Chuo hicho kitakuwa mjini Bamako, Mali.

akon 4
Wananchi wakifurahia umeme uliosambazwa kupitia mradi wa Akon

Akon Lighting Africa imepokea mkopo wa dola bilioni 1 kutoka kampuni ya China ya Jiangsu International.

akon 5

akon 9

akon 1

akon 6

akon 8

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents