Habari

Tazama picha za matukio mbalimbali yaliyojiri bungeni leo May 15, 2018

Kikao cha 29, mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea Bungeni mjini Dodoma muda huu, likiwa limeongozwa na Mwenyekiti wa Bunge,Andrew Chenge, ambapo kipindi cha maswali na majibu kimeendelea; Tazama matukio katika picha


Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akijibu miongozo mbalimbali ya wabunge leo Bungeni Jijini Dodoma


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Mhandisi Isaac Kamwelwe wakati wa kikao cha ishirini na tisa cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma


Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Dk.Adelardus Kilangi wakati wa kikao cha ishirini na tisa cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma


Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Charles Tizeba akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019


Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Dk.Adelardus Kilangi akiteta jambo na Mbunge wa Vunjo Mhe.James Mbatia wakati wa kikao cha ishirini na tisa cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents