Burudani

Tazama picha za warembo 20 watakaowania taji la Miss Rwanda 2018

Jana usiku wa kuamkia leo Jumapili Februari 4, 2018, kulikuwa na mchujo wa kuwapata warembo 20 ambao watafuzu katika hatua za mchujo wa kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha Miss Rwanda 2018.

Warembo 20 watakaochuana kwenye shindano la Miss Rwanda 2018.

Ikiwa ni tofauti kidogo na Tanzania katika hatua za mchujo, Warembo hao walianza kwa  kuulizwa maswali na jopo la majaji ambapo kulikuwa na wasichana 35 walioshinda kutoka kwenye mikoa mbalimbali nchini humo hadi kupata washiriki 20.

Jopo hilola Majaji limeundwa na majaji watatu ambao ni pamoja na Miss Rwanda namba mbili mwaka 2009 Rusaro Carine, Mtangazaji wa Kiss FM Sandrine Isheja Butera na Francine Uwera Havugimana kutoka shirikisho la taasisi binafsi.

Matokeo ya ushindi wa warembo hao yamepatikana kwa kuangalia urembo (maksi 30), majibu ya maswali waliyoulizwa (maksi 40) na ustadi wa kujibu maswali (maksi 30) na kilele cha mashindano hayo ni Tarehe 24 Februari, 2018 na sherehe zitafanyika katika ukumbi wa Kigali Convention Centre.

Tazama picha za warembo hao na majina yao;

Solange Uwineza
Paula Umutoniwase
Belinda Uwonkunda
Divine Ingabire
Belinda Ingabire
Lydia Dushimimana
Anastasia Umutoniwase
Vanessa Irakoze
Fiona Uwase
Rebecca Umuhire
Liliane Iradukunda
Noriella Ishimwe
Karen Umuhoza
Shemsa Munyana
Irene Natasha Ursule
Shanitah Munyana
Liliane Uwase Ndahiro

Picha kwa hisani ya Mtandao wa Inyarwanda

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents