Habari

Tazama picha za yaliyojiri bungeni leo katika kikao cha 34

Kikao cha 34, mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea Bungeni mjini Dodoma muda huu, likiwa limeongozwa Spika wa Bunge,Job Ndugai,Ambapo kipindi cha maswali na majibu kiliendelea; Tazama matukio katika picha


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma


Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akitolea ufafanuzi kuhusu hitaji la magari katika vituo vya polisi leo Jijini Dodoma


Wabunge wa Viti Maalum Mhe.Munira Mustafa Khatib na Mhe.Halima Abdallah Bulembo wakifurahia jambo wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso akieleza mipango mbalimbali ya wizara yake katika kutatua changamoto za miradi ya maji wakati wa kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma


Mbunge wa Lupa Mhe.Victor Mwambalaswa akiuliza swali wakati wa kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.William Ole Nasha wakati wa kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk Augustine Mahiga akizungumza jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Hamisi Kigwangalla na Naibu wake Mhe.Japhet Hasunga wakati wa kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents