Michezo

Tazama Ujerumani walivyowasili uwanja wa ndege baada ya kutolewa kombe la dunia (+Picha)

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low akiwa sambamba na kikosi chake wametua nchini kwao asubuhi ya leo baada ya kuyaaga mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea huko Urusi.

Mabingwa hao watetezi wametolewa baada ya kukubali kipigo kutoka kwa timu ya taifa ya Korea Kusini kwa jumla ya mabao 2 – 0 hapo jana siku ya Jumatano.

Kwakutambua kuwa wamewakwaza Wanaujerumani wengi waliyokuwa na mapenzi mema na timu yao kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter Ujerumani imewaomba radhi mashabi wake wote duniani kwa kutolewa mapema.

Picha za matukio baada ya kikosi cha Ujerumani kutua uwanja wa ndege

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents