Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Tazara yazidi kuchungulia kaburi

MAMLAKA ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) inaendelea kukumbwa na matatizo makubwa kibiashara kufuatia injini za treni na mabehewa ya kusafirishia abiria na mizigo kuzidi kupungua.

Na Editha Majura

 

MAMLAKA ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) inaendelea kukumbwa na matatizo makubwa kibiashara kufuatia injini za treni na mabehewa ya kusafirishia abiria na mizigo kuzidi kupungua.

 

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Meneja uhusiano wa Tazara,Conrad Simuchile, zinaeleza kuwa shirika hilo linaendelea kukabiliwa na ukata wa fedha unaosababishwa na kushindwa kufanya biashara katika kiwango kinachotakiwa kutokana na uhaba wa vitendea kazi hivyo.

 

Alisema mizigo inayohitaji kusafirishwa ni mingi isipokuwa wanashindwa kutokana na kukosa vitendea.

 

Simuchile alisema tatizo hilo lilianza muda mrefu na kwamba wana hisa wa mamlaka hiyo ambao ni Serikali ya Tanzania na ya Zambia wameisha elezwa hali halisi.

 

Hali mbaya ya Tazara haijaanza leo, ingawa kwa sasa imekuwa mbaya zaidi. Hunahitajika vitendea kazi vipya vinginevyo mamlaka inaweza kufa. Wana hisa wanafahamu hali hii kwani wali ishaelezwa na uongozi na wao waliahidi kuliyatafutia ufumbuzi matatizo hayo,� alisema Simuchile.

 

Alisema Tazara inategemea biashara ya kusafirisha mizigo ili iendeshwe kwa faida, alisema zaidi ya asilimia 95 ya mapato yake yanategemewa kutokana na usafirishaji wa mizigo si abiria. Lakini alisema hawawezi kutoa kipaumbele kwa mizigo pekee kwa sababu huduma ya kusafirisha abiria inategemewa na jamii.

 

Alisema kwa kuzingatia hilo, hulazimika kugawa mabehewamachache yaliyopo kuhudumia abiria pamoja na mizigo, hali ambayo alisema ni vigumu kwa mamlaka kuendeshwa kwa faida.

 

Simuchile alisema Tazara ilitakiwa kuwa na angalua injini 20 na mabehewa 2,000 tofauti na sasa ambapo ina injini zisizozidi kumi na moja na mabehewa 1,200.

 

Alisema ni vigumu kupata faida wakati kuna upungufu wa mabehewa 800. Hata hivyo alisema wanahisa waliahidi kutekeleza hatua zitakazoondoa tatizo hilo.

 

Oktoba mwaka jana Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, pamoja na vitu vingine ilitoa msaada wa mabehewa 50 kwa Tazara. Msaada huo kwa ujumla ulikuwa na thamani ya dola za Marekani 4.5 milioni 4.5 (sawa na zaidi ya sh. bilioni tano).

 

Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa China kuisaida Tazara, awali mwaka juzi ilitoa msaada wa vitendea kazi mbalimbali vilivyokuwa na thamani ya dola 12 Marekani milioni.

 

Source: Mwananchi

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW