TBC wajipanga

TBC wajipanga
Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, lipo mbioni kufanya ukarabati wa
studio zake na miundo mbinu katika kuhakikisha mashabiki wa kandanda
nchini wanapata matangazo ya moja kwa moja ya michuano mbalimbali ya
Fifa ikiwemo Kombe la Dunia katika ubora wa hali ya juu

Mkurugenzi wa TBC, Dunstan Tido Mhando alisema alipokuwa akijibu
maswali ya waandishi wa habari katika mkutano alioitisha juzi kutangaza
TBC kupewa haki ya kurusha matangazo ya Fainali za Kombe la Dunia 2010
kupitia vituo vyake vya redio na televisheni.

‘‘Tuthakikisha msisimko wa Kombe la Dunia na michuano mingine
inawafikia Watanzania vizuri kwa ubora wa hali ya juu, tunajua tatizo
letu kubwa ni la kiufundi linatokana na studio kutofanyiwa ukarabati
tangu zilipojengwa. Tumepata fedha kutoka serikalini, usikivu utakuwa
bora kuliko vituo vyote,’’ alisema Mhando.

Alifafanua kuwa kasma hiyo ipo katika bajeti yao ya kawaida kutoka
serikali kuu ambayo imezitoa ikitimiza wajibu wake kwa chombo hicho cha
umma.

‘‘Tuna hakika hadi mwakani tutakuwa bora, tutafanya marekebisho makubwa
Watanzania watapata uhondo kushuhudia Kombe la Dunia kupitia TBC pekee.

Tumepewa haki ya kuonyesha Kombe la Dunia, Kombe la Shirikisho na
michuano mingine ya Fifa kupitia Chama cha Watangazaji wa Afrika,
hatukushindanishwa, vigezo wanajua wenyewe,’’ alisema bosi huyo wa TBC.

Kuhusu matatizo ya upatikanaji usioridhisha wa televisheni ya TBC1
kwenye baadhi ya maeneo nchini Tido alisema ofisi yake inafahamu sababu
yake na kuwa inatafuta

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents