Habari

TBL yashinda tuzo ya kizibo cha dhahabu, kuonyeshwa kwa Watanzania

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imepata Tuzo ya Kizibo Cha Dhahabu inayomaanisha Ubora wa Kimataifa kutokana na uzalishaji wa bidhaa zake bora.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Brand za TBL, Pamela Kikuli alisema kuwa, TBL imefurahi kupata tuzo hiyo ambayo alisema kuwa imeongeza heshima katika jina la kampuni na bidhaa zake na kwamba wataendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kukidhi mahitaji ya wateja wake nchini kote.

“Kwakweli tumefurahi sana kupata tuzo hii ambayo ni ya kimataifa. Kila mara tunafikiria kuendelea kuwa vinara katika soko. Ndiyo maana bidhaa zetu zinakuwa na ladha na ubora wa kimataifa vitu ambavyo vinawavutia wateja wetu katika soko la Tanzania.” Aliongeza.

Bi. Pamela alisema pia kuwa, kwa kuwathamini wateja wake tuzo hiyo itapelekwa katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili kuwapa fursa ya kushuhudia tuzo hiyo.

Kwa mujibu wa Kikuli, tuzo hiyo siku ya Jumatano, Februari 26, 2020 itaoneshwa makutano ya barabara katika eneo la Mbagala Rangi Tatu kuanzia saa 8:30 mchana hadi saa 1:00 jioni ambapo wateja mbalimbali na wananchi kwa ujumla watapata fursa ya kuigusa tuzo hiyo na hata wengine kupiga nayo picha.

“Baada ya Mbagala, siku ya alhamisi tarehe 27 kizibo chetu cha dhahabu kitaoneshwa makutano ya barabara ya Karume, Ilala kuanzia saa 1:00 kamili asubuhi hadi 8:00 mchana kisha kuelekea eneo la Biafra, Kinondoni na kuoneshwa kuanzia saa 9:00 mchana hadi saa 1:00 kamili jioni. Ziara ya maonesho ya kizibo itaishia siku ya Ijumaa, tarehe 28 katika eneo la makutano yabarabara eneo la makutano ya barabara Buguruni kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 1:00 jioni.Lengo letu ni kusherehekea na wateja wetu ambao ndiyo wametufikisha hapa tulipo,” alisema
Kikuli.

Bidhaa zinazozalishwa na TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Light, Castle Lager, Castle Milk Stout, Redds Original, Budweiser, Balimi Extra Lager, Eagle Lager, Grand Malt na Safari Sparkling Water. TBL group imeorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam, ikiwa na wafanyakazi takriban1,700, inafanya uzalishaji katika mikoa minne ikiwa na vituo kadhaa vya usambazaji wa bidhaazake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents