Habari

TBS kuundwa upya,vijana 136 kupata shavu la ajira

Serikali imesema italiunda upya shirika la viwango nchini TBS na kutengeneza menejimenti mpya ili kuongeza ufanisi wa utendaji katika shirika hilo huku wakianza kutafuta vijana 136 watakao waajiri.

charles-mwijage

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa utoaji wa tuzo kwa washiriki wa Programu ya Kaizen iliyo chini ya shirika la maendeleo la kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

Alisema lengo la kuiunda upya TBS ni kuhakikisha kwamba kazi zinafanyika ipasavyo ili kulinda viwanda vya ndani, vinavyozalisha bidhaa mbalimbali.

“Na ndio maana mimi naongeza nguvu na ntaongeza nguvu na nimeomba serikali  tayari wanipe vijana 136. Work force niliyonayo inafanya kazi inataka watu zaidi na ntaiunda upya TBS,nitatengeneza upya menejimenti,ntaajiri vijana 136 tutakwenda kazini ndiyo biashara yenyewe,”alisema Mwijage.
BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents