Technology

TCRA: Kiama cha simu feki ni leo

‘Marehemu alikuwa mtiifu na alinipa michongo mingi enzi za uhai wake,’ watu wengi wanaomiliki simu feki watajikuta wakisema kauli hii Alhamis hii, June 16.

real-vs-fake

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA imesisitiza kuwa zoezi la uzimwaji simu feki unatekelezwa leo kama ilivyokuwa imepangwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, James Kilaba alisema kwa wale watakaofanya ujanja wa kubadilisha namba tambulishi (IMEA) watachezea kifungo cha miaka 10 jela au faini ya shilingi milioni 30 au vyote.

“Simu bandia zimepungua hadi chini ya asilimia 5! Hakuna kuongeza muda. Simu bandia ukomo wake pale pale 16 Juni,” TCRA wametilia mkazo kwenye Twitter.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents