Habari

TCRA na Jeshi la Polisi kula sahani moja na wezi wanaotumia mitandao ya simu

Serikali imesema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na Polisi watahakikisha wanafanya kazi kwa ukaribu kuhakikisha wote wanaotapeli kwa njia ya mitandao wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kali za kisheria.


Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali akiuliza swali leo Bungeni jijini Dodoma

Hayo yamebainishwa na kupitia Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, Bungeni Jijini Dodoma Wakati akijibu swali la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali aliyehoji; “Kumekuwa na wimbi sasa limeibuka la wizi wa kutumia mitandao ya simu wakiwa wanatuma sms kuwa umeshinda ‘Tatu Mzuka’ mara umeshinda Tigo, tuma pesa kwenye namba hii,kumekuwa na desturi hiyo sasa hivi. Nilitaka kupata majibu kutoka kwa Waziri TCRA imechukua juhudi gani wizi wa kutumia simu kwenye mitandao unakomeshwa na kuhakikisha wahusika wanakamatwa?


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akijibu swali la Mh. Bobali leo Bungeni Jijini Dodoma

“Ni kweli kwamba kumekuwa na matukio ya kutumiwa sms Watanzania mbalimbali ambazo zinaonyesha viashiria kwamba kuna utapeli unaoendelea katika huduma za mawasilino lakini kwa kutumia sheria ya 2015 ya wizi wa mitandao TCRA kwa kushirikiana na Polisi wameendelea kufanya kazi kwa karibu kuhakikisha kwamba wote wanaosambaza ujumbe huo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,” amesema Nditiye.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents