Habari

TCRA: Tanzania yafikisha watumiaji wa internet milioni 5.9

Hii ni habari njema kwa wafanyabiashara ya mtandaoni kwakuwa wana uhakika wa kuendelea kuwafikia wateja wengi zaidi wakati wa kutangaza bidhaa zao na tena kwa gharama nafuu.

social-media-pack-1

Kwa mujibu wa ofisa wa Idara ya Maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa TCRA, Connie Francis, watumiaji wa internet nchini wamefikia milioni 5.9.

Gazeti la Mwananchi la leo limeripoti kuwa idadi hiyo imeongezeka kutoka watu 26,000 mwaka 2000 hadi watu milioni 5.9 kwa mujibu wa takwimu za June mwaka jana. Kuna uwezekano mkubwa kuwa idadi hiyo imeongezeka kwa kasi zaidi mwaka huu.

Francis alitoa takwimu hizo jijini Mbeya wakati wa semima ya ya wadau wa mtandao wa internet iliyohusisha uundaji wa kamati ya mpito ya ya uanzishwaji wa kituo cha Mbeya Internet Exchange Point.

Kutokana na kuongezeka umuhimu wa internet katika shughuli za kibiashara, kiuchumi na kijamii, TCRA imeamua kuanzisha mradi utakaowasaidia watumiaji wa internet nchini kupata huduma hiyo kwa ubora, urahisi na haraka zaidi na kwa gharama nafuu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents