Habari

TCRA yaichimba mkwara Star TV, yaiamrisha kurudisha signal Startimes, Star TV yaendelea na msimamo wake

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA leo imekiamrisha kituo cha runinga cha Star TV kirudishe matangazo yake iliyoyakatiza weekend iliyopita kupitia king’amuzi cha Startimes.

ITV

Akiongea na waandishi wa habari leo, mkurugenzi mkuu wa TCRA Profesa John Nkoma amesema Star TV na Star Media wanatakiwa kuzingatia masharti yaliyoanishwa kwenye leseni zao.

Msikilize hapo chini.

Kutokana na hatua hiyo, Profesa Nkoma aliitaka Star TV kurudisha matangazo hayo kuanzia leo, uamuzi ambao hadi sasa haujanywa na kituo hicho.Alisema kama kuna matatizo, Star TV inapaswa kuwasiliana na TCRA ili kuyatatua.

Inadaiwa kuwa mwanasheria wa king’amuzi cha Continental kinachomilikiwa na kampuni ya Sahara ya Media Group alituma barua ya kuitaarifu startimes kujitoa kwa Star TV.

Baadaye Startimes walitoa ujumbe uliokuwa ukipita kwenye screen usemao: Ndugu mteja kutokana na matakwa ya STAR TV inatulazimu kuitoa katika orodha ya chaneli zetu. kwa maelezo zaidi piga STAR TV 0202503262. Samahani kwa usumbufu utakao jitokeza.

Hata hivyo mpaka muda huu Star TV haijarudi hewani kwenye king’amuzi hicho. Sababu za Star TV kujitoa zinadaiwa kuwa pamoja na kutopata faida yoyote kuwa kwenye king’amuzi hicho.
Kuna tetesi kuwa ITV nayo imepanga kufanya hivyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents