Promotion

Tecno Boom 7 ni simu kali kwa kijana anayependa muziki, picha, video na mitandao ya kijamii

Tecno imezindua kwenye soko la smartphones simu zake mpya zinazowalenga zaidi wapenzi wa muziki. Simu hizo zinaitwa Boom J7!

10995303_887987664578379_772900016624881400_n

Kabla sijakueleza vitu vya kuvutia kwenye simu hii ningependa kukueleza kwa ushahidi wa macho yangu mwenyewe kuwa Boom J7 ni simu zilizotengenezwa kwa muonekano wa theme za kuvutia na muonekano wa icons kwenye kioo chake utayavutia mno macho yako.

Tecno Boom J7 inakuja na kioo cha touch screen ambayo ni Full HD ya 5.0. Zinakuja zikiwa na rangi mbalimbali kwendana na mapenzi yako. Rangi hizo ni pamoja na kijivu, nyeusi, nyeupe, pinki na kijani.

tecno

Ndani ya kibox!

Ukinunua simu hii kwa mara ya kwanza utaikuta ikiwa kwenye kibox kizuri chenye umbo la mraba ambamo ndani yake utakutana na simu yenyewe pamoja na vibox vingine vidogo vilivyo na vifaa vingine muhimu.

Tecno-Boom-J7-005-Techweez

Ndani yake utakuta umewekewa ‘case’ mbili za rangi tofauti za kuivalisha simu yako. Kwa maana hiyo hapo utakuwa umeokoa tayari takriban shilingi 40,000 ya kununua case ya kuvalisha simu yako.

Tecno-Boom-J7-003-Techweez

Mimi kwa upande wangu nimeipenda ile yenye rangi nyeusi iliyofifia na ndio nimeivalisha simu yangu. Kuna nyingine ya rangi ya blue bahari ambayo nahisi inawafaa zaidi akina dada.

Boom J7 ni simu laini na inayoteleza vyema mkononi na hiyo ni sababu ya wembamba wake na upana wa kutosha mkononi. Ile kesi ya kuilinda simu yako inaifanya simu yako ishikike vyema zaidi mkononi.

Hautokutana na screen protector ndani ya box kwakuwa simu hiyo tayari inakuwa imewekwa kwenye screen hivyo unaweza kuendelea kuitumia bila hofu. Haikwanguki kirahisi pia.

Betri yake ina nguvu ya 2020mAh, earphones za kuvutia zikiwa zimewekwa kwenye kipochi chake maalum pamoja na kikaratasi kidogo cha waranti ya miaka miwili. Kwa ukubwa wa betri hiyo una uhakika wa kukaa na chaji kwa muda mrefu na kwa matumizi bora na kucheza na power-saving mode utafurahia simu hii bila kuwa na wasiwasi wa kuzimikiwa njiani.

Nimekaa na simu hii kwa zaidi ya siku nne sasa kama simu yangu ya kutumia kuanzia kupiga na kupokea simu, kutuma sms, kutumia WhatsApp, Instagram, Twitter na mitandao mingine na ninakuhakikisha kuwa hii simu ni bomba mbaya!

20150513074411
Boom J7 inatoa picha bomba

Display yake ya inchi 5 yenye HD inakufanya ubrowse website zako uzipendazo. Kwa resolution ya 720 x 1280, simu hii inakufanya uone picha na video katika muonekano wa kuvutia sana. Nenda Youtube angalia video uipendayo utashangaa video zinavyoonekana kwa quality ya hatari! Maandishi yanavyoonekana ndio usiseme!

Ina camera mbili, ya nyuma ikiwa na 8.0 megapixels na ile ya mbele ikiwa na 2.0MP na zote zikiwa na auto focus. Uwezo huo unakuhakikishia picha na video za kuvutia.

20150513073717
Picha niliyopiga na simu yangu ya Tecno Boom J7

Ukubwa wake ni 1GB RAM + 16GB ROM na unaweza kuongeza kadi hadi yenye uwezo wa kubeba 32GB. Boom J7 inatumia lini mbili, ya kawaida na Micro.

Nguvu ya Processor Je?

Simu hii ina processor ya 1.3GHz Quad Core ikitumia mfumo wa Android 4.4.2.

Tecno Boom J7 ina ram yenye ukubwa wa 1GB yenye uwezo wa kuifanya simu yako ifanya kazi kwa speed inayoridhisha kabisa.

Unaweza kuiita simu ya muziki, Tecno Boom J7 imetengenezwa katika mfumo ambao muziki utausikia kwa sauti uliyoitaka kwa kipindi kirefu. Hivyo kama unapenda muziki, basi ni lazima utaipenda CNO BOOM J7.

11182070_885744608136018_3905683619155817010_n

Furahia, #‎ItsBoomTime…

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents