Technology

TECNO CAMON 16s kuingia sokoni hivi karibuni

Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO inatarajia kuzindua simu mpya ya TECNO CAMON 16s, ni simu ambayo inakuja na teknolojia kubwa ya kamera na uwezo mkubwa  utakaowanufaisha watumiaji katika shughuli zao za kiofisi na kiuchumi.

Taarifa kutoka kampuni ya TECNO zinaeleza kuwa TECNO CAMON 16s ina kamera nne nyuma na kamera kuu ikiwa na 48MP.

Kamera hiyo yenye uwezo wa kuchukua picha ang’avu bila kujalisha mazingira au muda ambao picha inapigwa hata kwenye mwanga hafifu simu hiyo ina uwezo wa kupiga picha ang’avu kuotkana na flashi zake nne za nyuma pamoja na lensi yenye teknolojia ya AI ambapo vyote kwa pamoja vinamsaidia mtumiaji wa simu hii kupata picha ang’avu hata kwenye mazingira yenye mwanga hafifu.

Pamoja na kuwa na kamera kubwa yenye uwezo, pia simu hiyo imedokezewa kuwa ina memori kubwa inayofikia GB 128 ROM kwa GB 4 RAM.

Ukubwa wa memori ya simu hii utamsaidia mtumiaji kuhifadhi vitu vyake bila kufuta pia kuiwezesha simu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi bila kukwama.

Vilevile simu hiyo ya TECNO CAMON 16s ina Skrini kubwa ya inchi 6.6 itakayompa mtumiaji furaha na uhuru wa kutazama video, kucheza gemu pamoja na kupiga picha zinazojitosheleza na kuenea vizuri kwenye screen ambazo zitakuwa zinaleta uhalisia wa picha halisi.

      Mwonekano wa wa ukubwa wa inchi 6.6” skrini ya TECNO CAMON 16s

Kufahamu zaidi ujio wa simu hii bofya link kwenda kwenye ukurasa wao wa Instagram;

https://cutt.ly/VgDoVDQ

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents