Technology

Tecno kuzindua Spark 5pro yenye memory kubwa

Soko la simu limekuwa na ushindani mkubwa na kupelekea makampuni ya kuja na mbinu mpya za kujizolea wateja. Tukiongelea makampuni pendwa ya simu hatuezi kuacha kuipongeza kampuni ya simu ya TECNO. TECNO imekuwa kampuni bora kutokana na utofauti wa bidhaa zake Spark ya sasa hauezi ilinganisha na Spark ijayo ndivyo mawazo yangu yanavyoniambia.

Tunafahamu TECNO inamatoleo mbalimbali kama vile phantom, Camon, L series, Spark Series na mengineyo, na yote ni matoleo pendwa kutokana kuwa na sifa zenye kuvutia kama vile kamera nzuri, battery kubwa. lakini kati ya matoleo yote toleo la Spark limeonekana kupendwa sana labda hii ni kutokana muonekano mkubwa, utendaji maridhawa na bei isiyomuumiza mteja.

Pengine msomaji unaweza jiuliza kwanini nimeamua kuizungumzia TECNO au kama vijana wamjini mnasema kupiga debe hahahahahha, sawa basi acha nipige debe, leo nikiwa katika pita pita zangu mitaa ya kariakoo, katika duka Fulani hivi linafahamika kwa jina la Electrophones nimemsikia mteja mmoja akitamba TECNO Spark 5pro mbioni kuja mbona tutaepukana na ununuzi wa vimemory vilivyo jaa virusihayo ma GB 64 yatanitosha kabisa kuhifadhi mavideo na mapicha picha.

Mh! nikiwa kama kijana mwenye kupenda utandawazi ndipo nilipo fukunyua kwenye ukurasa wa IG @tecnomobiletanzania na kukutana na picha ya Spark 5pro yenye sifa zenye kuonekanika kama kioo aina ya Dot in Display cha takribani nchi 6 au 7 si chini ya hapo, nyuma ikiwa na kamera 4(16MP+2MP+2MP+AI Lens) na MP8 za selfie. Kutokana na sifa hizo chache TECNO Spark 5pro ni mkali wa Spark zote za awali.

Ili kufahamu mengi zaidi tembelea mara kwa mara ukurasa wa Instagram @tecnomobiletanzania .

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents