Promotion

Tecno watimiza ndoto za watoto yatima Dar Es Salaam (+video)

Katika kuhakikisha jamii ya Kitanzania inafanikiwa na kufaidika kwa uwepo wake kampuni ya simu nchini Tanzania TECNO Mobile yahakikisha zaidi ya watoto 100 ambao ni yatima wanapata vifaa vya shule.

TECNO imefanikiwa kuchangia fedha pamoja na mahitaji mengine ya msingi kwa kituo cha Chanika Children Shelter kinacholea watoto yatima kilichopo chanika, jijini Dar es salaam, katika kituo hicho takribani watoto wenye umri tofauti kuanzia miaka 4 mpaka 18 wanalelewa kwa usaidizi mkubwa wa mmiliki wa kituo hiko kiongozi wa madhehebu ya budha nchini Dr. Pannasekara.

Akizungumza wakati wa makabidhiano meneja wa uhusiano wa kampuni ya simu ya TECNO bwana Erick Mkomoye alisema kwamba, “ndoto za Watoto hao ndio zilizopelekea kampuni ya simu ya TECNO kuanzisha kampeni inayofamika KUWA SHUJAA WANGU na kuanzia kwa kuchangia hundi ya kiasi cha millioni 5 ili kutimiza mahitaji yao ya shule, tuliwashawishi watanzania na wateja wetu kuwasaidia watoto hawa kadri wawezavyo lakini pia sisi kama kampuni pia tutawasaidia watoto hawa kuhakikisha ndoto zao zinatimia tumeanza na million 5 na tutaendelea. ”

Bwana Eric aliongeza, “KUWA SHUJAA WANGU ni kampeni ambayo imepelekea kuwasaidia watoto wa Chanika Children Shelter ili kutimiza ndoto zao za kwenda shule na kuanza masomo yao katika ngazi tofauti tofauti sekondari na msingi na hata chekechea ili baadae waje timizia ndoto kubwa zaidi za kuwa daktari, mwalimu, rubani katika kulifanikisha hili TECNO tumeamua kuipa muendelezo kampeni hii kwa mwaka wote huu wa 2019”.

Alimaliza,na baadhi ya vitu vyengine ambavyo kampuni imefanikiwa kuviwasilisha Chanika Children Shelter ni mafuta, mchele, unga, sukari, sabuni kwaajili ya matumizi ya kila siku.
Kituo cha Chanika Children Shelter kinatunza watoto zaidi mia moja wenye umri tofauti tofauti wanaofika wenyewe au kuletwe kutokana na mazingira magumu wanayokumbana..

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents