DStv Inogilee!

TECNOLOJIA: Nunua toleo jipya la Tecno Camon 11 kwa kubadilishana na matoleo ya zamani ya Camon Series (+video)

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kushirikiana na Tecno wamezindua simu mpya ya Tecno Camon 11 na kutangaza habari njema kwa wateja wao, kwamba watanunua simu hiyo kwa kubadilishana na simu za matoleo ya zamani ya Camon Series.

Mkuu wa kitengo cha uhusiano na mawasiliano (kati) Jacqueline Materu pamoja na Meneja uhusiano kutoka @TecnomobileTZ Bw. Eric Mkomoya wakionesha simu hio ya Tecno Camon 11 kwa waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi simu hiyo leo Desemba 5, 2018 jijini  Dar Es Salaam, Meneja masoko wa Kampuni ya Tecno, Erick Mkomoya amesema “Tmedhamiria kuhakikishia kuwa kila Mtanzania anamiliki simu janja na kwa pamoja tunalifanya taifa letu liwe la kidijitali,”.

Ujio wa Ofa hii utawafanya Watanzania waweze kubadilisha simu zao na kupata toleo hilo jipya la simu. Mabadilishano hayo ni kwamba utapata punguzo kutoka Tsh 400,000/= ya bei ya Toleo jipya la Camon 11 na mapunguzo yametofautiana kutokana na aina ya toleo lako la zamani la Camon Series.

Kingine kizuri ni kwamba, simu hiyo ya Camon 11 itakuja na GB 15 za kuperuzi ambazo kila mwezi mteja atapewa GB 5 za kuperuzi, ambazo zitadumu kwa miezi mitatu.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW