Burudani

Tekno kwa Diva: Wewe ni msichana mrembo kwanini huna mpenzi?” Sikiliza mahojiano yao ya kuvutia hapa (Audio)

Kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM kinachoendeshwa na Diva The Bawse kimeendelea kuvuka boda.

diva

Siku za hivi karibuni mtangazaji huyo maarufu amekuwa akihoji wasanii wengi wa nje ya Tanzania wakiwemo Iyanya, Patoranking, Maurice Kirya na sasa amezungumza na hitmaker wa Duro, Tekno Miles wa Nigeria.

Kwenye mahojiano hayo Diva amemuuliza staa huyo kuhusu issue za muziki na ofcource kuhusu malavidavi. Hata hivyo kabla ya kujibu swali, Tekno aliamua kugeuka mtangazaji kwa muda na kumbananisha Diva kuhusu maisha yake ya mahaba.

“Do you have a boyfriend,” alihoji muimbaji na producer huyo wa Nigeria. “No, I am not dating, I don’t have a boyfriend,” alijibu Diva. “Why? You are very hot, you should have a boyfriend,” alichombeza Tekno. “I am hot?” Diva aliuliza kana kwamba masikio yake yamemdanganya kwa kile alichosikia. “Yes, I see a lot of fans love you in Tanzania, you should be taken right now,” aliongeza Tekno.

Diva alijibu kuwa kwa sasa anapenda kuwekeza akili na nguvu yake kwenye kazi yake zaidi. “I don’t have a boyfriend, very serious, I am just single, I am busy working,” alisisitiza.

Hata hivyo kwa upande wake Tekno kama ilivyo kawaida kwa wasanii wengi maarufu, alisema hana mrembo yoyote na kueleza kuwa ‘I am in love with my music.’ Hata hivyo alikiri kuwa wanawake wengi wanamtaka wavunje naye amri ya sita japo amekuwa akiwachomolea bila huruma!

Sikiliza mahojiano hayo hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents