Soka saa 24!

Teknolojia ya VAR kufanyiwa majaribio mechi hizi tano za EPL Jumamosi

Teknolojia ya VAR kufanyiwa majaribio mechi hizi tano za EPL Jumamosi

Teknolojia ya kutumia video kuwasaidia waamuzi, maarufu kama VAR, itafanyiwa majaribio katika mechi kadha kwa pamoja Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza Jumamosi.

Brighton & Hove Albion’s Yves Bissouma battles with Liverpool’s Naby Keita during the Premier League match at Anfield Stadium, Liverpool. Picture date 25th August 2018. Picture credit should read: Matt McNulty/Sportimage via PA Images

Teknolojia hiyo itajaribiwa katika mechi tano ambazo zitakuwa zinachezwa kuanzia saa kumi na moja saa za Afrika Mashariki.Baada ya kujaribiwa katika mechi moja moja msimu uliopita, wasimamizi wa Ligi ya Premia sasa wanataka kuona iwapo teknolojia hiyo inaweza kufanikiwa ikitumiwa katika mechi kadha kwa wakati mmoja.

Majaribio hayo yatakuwa yanadhibitiwa kutoka kituo kimoja kikuu cha VAR.Hakutakuwa na mawasiliano ya aina yoyote na waamuzi uwanjani mechi zitakapokuwa zikiendelea.Kwa sasa wakati wa majaribio, teknolojia hiyo ya VAR itatumiwa katika uamuzi wa kuthibitisha magoli yanapofungwa, kuamua mikwaju ya penalti, kadi nyekundu za moja kwa moja na kuwatambua wachezaji wakati wa kutoa adhabu, hasa wanapokuwa wengi kwa pamoja kiasi cha kumkanganya mwamuzi.

Mechi ambazo VAR itafanyiwa majaribio ni:-

  • AFC Bournemouth v Leicester City
  • Chelsea v Cardiff City
  • Huddersfield Town v Crystal Palace
  • Manchester City v Fulham
  • Newcastle United v Arsenal

Aprili, klabu za Ligi ya Premia zilipiga kura dhidi ya kutumiwa kwa teknolojia hiyo msimu wa 2018-19.Sawa na msimu uliopita, VAR itatumiwa tu katika Kombe la EFL na Kombe la FA lakini katika viwanja vya klabu zinazocheza ligi kuu.Ilitumiwa katika mechi 1 msimu uliopita, na msimu huu inatarajiwa kutumiwa katika mechi takriban 60.

Chanzo BBC

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW