Uncategorized

Teknolojia ya Video ingekuwepo goli langu lisingekubaliwa – Maradona (Video)

Gwiji wa mchezo wa mpira wa miguu raia wa Argentina,Diego Maradona ameunga mkono utumiaji wa kanda za video licha ya kukiri kwamba bao lake la ”Hand of God” dhidi ya Uingereza 1986 halikufaa kukubalika.

Maradona alitumia mkono wake kufunga bao ambalo liliisaidia timu yake ya taifa ya Argentina kuchomoza na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Uingereza katika mchezo wa robo fainali ya kombe la dunia miaka 31 iliyopita.

”Kwa kweli mimi hukumbuka bao hilo kila mara ninapounga mkono matumizi ya teknolojia” ,Maradona aliambia Fifa.com. Nilifikiria kuhusu bao hilo na kwa kweli bao hilo halikufaa kuidhinihswa”amesema Maradona.

Maradona anasema kuwa alifaidika kutokana na ukosefu wa teknolojia katika kombe la dunia na haikuwa mara moja bali mara mbili.

”Nitakwambia kitu chengine -katika kombe la dunia la 1990 nilitumia mkono wangu kuondoa mpira uliokuwa karibu kuingia katika goli letu dhidi ya taifa la Usovieti. Tulikuwa na bahati kwa sababu muamuzi hakuona”.

Hii ni kutokana na kukosekana kwa teknolojia wakati huo lakini sasa ni mambo mengine”.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents