Michezo

Teknolojia ya video (VAR) kutumika rasmi kombe la dunia

Teknolojia ya video ya ‘Video assistant referees’ (VAR) inatarajiwa kutumika rasmi katika michuano ya kombe la dunia huko nchini Urusi baada ya Shirikisho la soka Duniani (FIFA) kuthibitisha hilo.

Teknolojia hiyo imekuwa ikitumika msimu huu katika michuano mbalimbali kama vile English cup, Ujerumani na Itali ikiwa kama sehemu ya majaribio

Rais wa Shirikisho la soka Duniani, Gianni Infantino amesema kuwa ni lazima tuishi kulingana na wakati.

Rais wa Shirikisho la soka Duniani, Gianni Infantino

Tunahitaji tuishi kulingana na wakati, ni lazima tuwapatie waamuzi wetu vifaa vyenye ubora ambavyo wataweza kufanya kazi kwa urahisi na kutoa maamuzi yaliyo sahihi na katika kombe la dunia hayo maamuzi yanahitajika.

Katika kombe la dunia 2018 kila mtu atashuhudia akiwa nyumbani kwake kwa dakika chache tu kama mwamuzi amekosea wakati akisahihishwa na teknolojia ya VAR.

Kwa mara ya kwanza teknolojia hii ya VAR ilitambulishwa katika michuano ya klabu bingwa duniani mwezi Desemba mwaka  2016 na kufanyiwa majaribio kombe la Shirikisho mwaka 2017.

Sistimu hii ilileta utata katika mchezo wa Tottenham ambapo waliibuka na ushindi  wa mabao 6 – 1 kombe la FA Cup dhidi ya Rochdale mwezi Februari wakati bao la penati lilipokataliwa.

Ligi kuu nchini Uingereza haitarajii kutumia mfumo wa VAR msimu ujao wakati Uefa tayari imeshasema kamwe haitatumia mfumo huo mwaka 2018-19 michuano ya Champions League.

Hispania na Ufaransa tayari imeshatangaza kuutumia mfumo huo msimu ujao wakati huko Bundesliga nchini Ujerumani wanatarajia kuutolea maamuzi Machi 22.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents