Habari

Tetemeko kubwa la ardhi laikumba Canada

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa Magnitude 5.8 limeikumba nchi ya Canada katika mji wa Montana.

Kwa mujibu wa mtandao wa US Today umeeleza kuwa tetemeko hilo lililoanzia mji wa Kusini mwa Lincoln limetokea mapema leo likiwa na urefu wa kilometa 9.7, hata hivyo hakuna aliyeripotiwa kupata madhara yoyote.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tetemekeo hilo ni kutokana na kuharibika kwa mitambo ya gesi iliokuwepo Helena, wameandika National Weather Service in Great Falls katiaka mtandao wao wa Twitter.

Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo, Ray Anderson ameliambia shirika la habari la AP kuwa tetemeko hilo lilikuwa ni kubwa sana katika maeneo ya Helena. Hata hivyo tetemeko hilo limeathiri maeneo ya Bozeman, Idaho na Great Falls.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents