Habari

Tetemeko la ardhi lauwa watu 6 nchini Italia

Watu sita wameripotiwa kufa kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea kwenye mji wa Accumoli na Pescara del Tronto nchini Italia.

_90895219_091172a5-fd38-46f4-85d5-8441d5f4717b

Mamlaka ya Marekani inayohusika na matetemeko ya ardhi USGS imesema tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na sita usiku saa za Italia (01:36 GMT), 76 km (maili 47) kusini mashariki mwa mji wa Perugia, katika kina cha 10km (maili sita) chini ya ardhi.

Tetemeko hilo linalokadiriwa kuwa na nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Ritcher limetikisa eneo la Umbria lililopo katikati ya Italia na kuwafukia watu chini ya vifusi, maafisa wa Italia wamesema.

Watu wanne wameripotiwa kufariki katika eneo la Accumoli huku wazee wawili wa mji wa Pescara del Tronto wameripotiwa kufa baada ya nyumba yao kuanguka, hiyo ni kwa mujibu wa Meya wa mji huo.

Gazeti la La Repubblica la nchini humo limedai kuwa tetemeko hilo limesikika kwenye miji mingi ikiwemo Roma, Perugia na miji mingine huku baadhi ya nyumba zikitikisika kwa muda wa sekunde 20.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents