Aisee DSTV!
SwahiliFix

TETESI: Fred kujiunga na Man United ndani ya masaa 24

Kiungo wa klabu ya Shakthar Donetsk na timu ya taifa ya Brazil, Frederico Santos maarufu kama Fred, anatarajiwa kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Manchester United ndani ya masaa 24 yajayo.

Mchezaji huyo amedaiwa kuondoka kwenye kambi ya timu ya Brazil kwa ajili ya kwenda kufanyiwa vipimo Jumatatu hii, kabla ya kutangazwa kuwa mchezaji mpya wa Man United.

Inadaiw kuwa usajili wa kiungo huyo mwenye mika 25, utajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 53.

Fred alikuwa anawindwa kwa ukaribu na Manchester City tangu dirisha dogo la usajili la mwezi January mwaka huu. Kiungo huyo alijiunga na Shakthar mwaka 2013 akitokea Internacional ya Brazil.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW