Tupo Nawe

RASMI: Hans Van Der Pluijm atimuliwa Azam FC, kipigo cha Simba champonza na huyu ndiye mrithi wake

Kocha mkuu wa klabu ya Azam FC, Hans Van Der Pluijm ametimuliwa kazi ya kuendelea kuinoa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Chamazi jijini Dar es salaam.

Mbali na Pluijm kocha msaidizi naye Juma Mwambusi amefungashiwa virago huku, Ettiene Ndayiragije wa KMC akitarajiwa kurithi mikoba hiyo kwa muda.

Kutimuliwa kazi kwa Pluijm kunatokana na muendelezo wa matokeo mabaya ya hivi karibuni kwenye mechi za ligi kuu soka Tanzania Bara.

Licha ya Azam kulazimishwa sare ya 1-1 na Coastal Union kwenye dimba la Mkwakwani Tanga lakini uongozi wa klabu hiyo ulivuta subira kuona kama kutakuwa na mabadiliko yoyote na ndipo wakakumbana na kipigo cha mabao 3 – 1 kutoka kwa Simba.

Hadi sasa Azam ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa na alama 50 baada ya michezo 25 wakati Yanga (wanaoongoza ligi) wana pointi 61 wakiwa wamecheza mechi 25 sawa na Azam.
Nyuma ya Azam ipo Simba (nafasi ya tatu) imecheza mechi 18 ina alama 45.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW