TETESI: Man United yapanga kuiharibia Man City kwa Sanchez

Klabu ya Manchester United inadaiwa kuingilia kati usajili wa Alexis Sanchez ambaye amekuwa anawindwa kwa ukaribu zaidi na majirani zao Manchester City.

Man United wamedaiwa kuwa wanataka kumsajili mchezaji huyo huku wakipanga kuliilipa Arsenal kiasi cha paundi milioni 25 pamoja na kumtoa mchezaji wao Henrikh Mkhitaryan kwenda kwenye timu hiyo.

Siku chache zilizopita ilidaiwa kuwa tayari City wameshamaliza mazungumzo na mchezaji huyo na kukubaliana mahitaji binafsi na kilichobakia ni kumaliza mazungumzo na Arsenal ambao walikuwa wanataka kiasi cha paundi milioni 35 kwa ajili ya kufanikisha usajili huo.

Man City walipanga kumlipa mchezaji huyo mshahara wa kiasi cha paundi 250,000 kwa wiki.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW