Michezo

TETESI: Mauricio Pochettino kurithi mikoba ya  Conte, Chelsea

Ikiwa ligi kuu nchini Uingereza tayari imefikia tamati kubwa ni hekaheka za usajili ambapo kwa hivi sasa kocha wa klabu ya Tottenham, Mauricio Pochettino anahusishwa kutua Chelsea ili kurithi mikoba ya Antonio Conte ambaye anatarajiwa kuondoka mara baada ya mchezo wake wa mwisho wa fainali ya FA atakapo wakabili Manchester United siku ya Jumamosi.

Chelsea imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao na hivyo Muitalia huyo kuondoka Stamford Bridge ikiwa imepita miezi 12 tu toka akipatie ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza kikosi hicho cha The Blues.

Klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la London imehusishwa pia kuwahitaji, Luis Enrique, Maurizio Sarri na hivi sasa Pochettino ili kuchukua mikoba ya Conte.

Chini ya Pochettino, Spurs imefanikiwa kufuzu michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa miaka mitatu mfululizo huku ikiwa inatumia bajeti ndogo ya fedha ukilinganisha na timu kama Manchester City, Manchester United, Liverpool, Chelsea na Arsenal.

Kocha huyo raia wa Argentina amesaliwa na miaka mitatu ya kuendelea kusalia Spurs huku kukiwa na mipango ya kuzungumza na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy kuongeza kitita cha fedha kwaajili ya usajili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents