Michezo

TETESI: Ndoto za Ibrahim Ajibu kutua TP Mazembe zayeyuka, Simba yahusishwa, Wakongo waitumia ujumbe Yanga kujiondoa

Wakati zikiwa zimebaki siku chache kabla ya ligi kuu soka Tanzania Bara kumalizika, klabu mbalimbali zimekuwa zikitumia muda mwingi katika kufanya usajili ambao utaziwezesha kuimarisha vikosi vyao huku wachezaji wengine wakizihama timu zao na wengine wakiongeza kandarasi.

Siku za hivi karibuni kulizuka taarifa kuwa miamba ya soka nchini DR Congo, TP Mazembe imehitaji huduma ya mchezaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu na kutuma barua ndani ya uongozi wa timu hiyo ili waweze kumsajili mara baada ya kumataba wake utakapo malizika mwezi ujao na kwenda kama mchezaji uhuru.

Katika tetesi hizo za usajili ni kuwa Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo imeghairisha mpango huo wa kumsajili mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajibu.

TP Mazembe imeiandikia email Yanga kujiondoka katika deal hilo baada ya kushindwa kukubaliana maslahi binafsi na Ajibu.

Mkataba wa Ajibu unamalizika mwezi ujao (June) na tetesi zimekuwa zikimhusisha kurejea kwenye klabu yake ya zamani Simba.

Hata hivyo taarifa zisizo rasmi kwenye  tetesi hizo za kutakiwa kusajiliwa kwa Ibrahim Ajibu zimeshindikana kutokana na klabu ya Simba kutaka kukaa meza moja na TP Mazembe kwaajili ya dili hilo kwakuwa miamba hiyo ya soka ya Msimbazi ilishafanya naye mkataba wa awali na mchezaji huyo.

 

Image result for Ibrahim Ajibu kwenda simba au tp mazembe

Inadaiwa kabla ya Mei 23 Meneja wa Ajibu aliwasiliana na klabu ya Simba kuwaaomba wamuruhusu Ajibu ajiunge na TP Mazembe kwa sababu alikuwa amesaini mkataba wa awali na klabu hiyo ndipo klabu ya Simba ikawaambia TP Mazembe waje kwenye meza ya mazungumzo kwa sababu wao wana mkataba wa awali na Ajibu na alishachukua baadhi ya fedha za usajili.

Simba wakawaambia TP Mazembe kuwa Ajibu anauzwa dola 100,000 ambazo ni zaidi ya milioni 220 za Kitanzania na kuwapa sharti la kuweka kwenye mkataba wake iwapo atauzwa klabu nyingine asilimia 20 ya mauzo yake wapate Simba. Ndipo TP Mazembe ikasitisha mpango wa kumsajili kwa sababu wenyewe walikuwa wanajua Ajibu ni mchezaji huru.

Image may contain: text

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents