Michezo

Tetesi: Vita kali Yanga SC, Azam FC kuinasa saini ya straika huyu dola milioni 1 kutengwa

Wakati duru la pili la ligi kuu soka Tanzania Bara linaelekea ukingoni huku baadhi ya timu zikijaribu kujinasua kutoka mkiani  kuepuka dhahama ya kushuka daraj, taarifa za chini zinaelaza kuwa klabu za Yanga na Azam FC zipo katika harakati za kunasa saini ya mchezaji wa Zambia, Chriss Mugalu.

Tokeo la picha la Chriss Mugalu best player

 

Taarifa za chini ya kapeti zinaeleza kuwa Mabingwa wa tetezi wa ligi kuu Tanzania Yanga SC  ipo kwenye mpango wa kunasa saini ya straika wa klabu ya Lukasa Dynamo, Chriss Mugalu ambaye huwenda ujio wake ukachukua nafasi ya wachezaji wake Doland Ngoma na Amissi Tambwe ambao wamekuwa wakisumbuliwa na majeraha mara kwa mara.

Yanga SC haipo peke yake kwenye vita hiyo bali  Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC inasemekana nayo inahitaji saini ya nyota huyo raia wa DR Congo na tayari imeshatenga kitita cha Dola 60,000 ili kumnasa.

Mugalu ambaye amekuwa mfungaji bora msimu uliyopita kwakufunga jumlaya mabao 20, mara kadhaa amehusishwa kutaka kuondoka ndani Lusaka Dynamo lakini timu hiyo imekuwa ikimng’ang’ania kwakuwa inahitaji kuwa miongoni mwa klabu bora Barani Afrika.

Hata hivyo Desemba 30 mwaka 2017 klabu ya Lusaka Dynamo inayoshiriki ligi ya ZSL ilitangaza kumuuza straika huyo kwa thamani ya Dola za Kimarekani milioni moja baada ya timu ya Zesco United kuhitaji kumsajili.

Hata hivyo Kocha Mkuu wa klabu ya Lusaka Dynamo Mzambia, Patrick Phiri  amewahi kusikika akisema kuwa Straika wake kamwe hawezi kuondoka.

” Kitu muhimu bado yupo nasi msimu huu, kitakacho tokea baada ya hapo hatutaweza kukizuia. Lusaka Dynamos haitoweza kumzuia mchezaji kama timu kubwa itakuja kumuhitaji.”  amesema kocha,Patrick Phir

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents