Michezo

TETESI: Yanga kumtimua kocha wao Mwinyi Zahera na kumnasa kocha huyu, Yeye ajibu tuhuma hizo – Picha

TETESI: Yanga kumtimua kocha wao Mwinyi Zahera na kumnasa kocha huyu, Yeye ajibu tuhuma hizo - Picha

Baada ya kichapo cha juzi dhidi ya Pyramids Fc ya Misri, inaelezwa kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mchakato wa kuachana na Kocha wao Mkuu, Mwinyi Zahera. Maamuzi hayo yanakuja si baada tu ya mechi ya jana bali pia katika mechi za Ligi Kuu Bara ambapo Yanga imeonekana kutofanya vizuri.

Tetesi zilizopo hivi sasa zinaeleza kuwa aliyewahi kuwa Kocha wa mabingwa hao wa Kihistoria, Mholanzi, Hans van der Pluijm, anaweza akarejea ndani ya timu hiyo muda wowote kuanzia sasa.

Hans aliinoa Yanga kwa mafanikio miaka ya hivi karibuni na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu mara kadhaa ambapo sasa anatajwa kutua tena Jangwani.

Hans mara ya mwisho alikuwa Kocha wa Azam FC ambayo ilimtimua mapema baada ya kuingia naye mkataba kutokana na kufanya vibaya kwenye mechi za ligi.

Lakini imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema hana wasiwasi endapo atafukuzwa kazi kunako klabu hiyo.

Taarifa imesema Zahera ambaye ni raia wa Congo ameeleza hana wasiwasi sababu ana ofa nyingi mezani ambazo anaweza akazitumia.

Ameeleza kuwa kufukuzwa ni sehemu ya kazi kwani makocha wengi huajiriwa na kufukuzwa hivyo kwake si jambo geni.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents