Michezo

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi hii, kipigo cha Liverpool kumuondoa, Coutinho Barcelona, Juventus kuachana na kocha wake, kinda wa Ajax, De Ligt aichomolea United

Mshambulaiji wa Brazil, Philippe Coutinho huwenda akawa mchezaji wa kwanza kuuzwa kutoka ndani kikosi cha Barcelona kufuatia kuondolewa kwa timu hiyo katika nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Liverpool.

Phillipe Coutinho

Coutinho mwenye umri wa miaka 26, alisajiliwa na Barcelona mwezi Januari mwaka jana kwa dau la pauni milioni 142 akitokea Liverpool.

Image result for Coutinho in bad emotion vs Liverpool 4 - 0

Bodi ya klabu hiyo pia inakutakana kuamua kuhusu hatma ya mkufunzi wa klabu hiyo Ernesto Valverde. (ESPN)

Kuzuiwa kusajili kwa klabu ya Chelsea ni habari mbaya sana kwa uhamisho wa mshambuliaji wa klabu hiyo na Ubelgiji Eden Hazard kuelekea Real Madrid na inaweza kuathiri uhamisho wa mchezaji huyo Uhispania. (AS)Eden Hazard

Juventus na kocha wake Massimiliano Allegri, 51, wanatarajiwa kuachana baada ya misimu mitano pamoja na mataji matano ya ligi alioshinda. Mkufunzi na mchezaji wa zamani wa Juve Antonio Conte amehusishwa kuchukua nafasi hiyo.. (La Stampa – in Italian)

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29. anataka kusalia katika klabu ya Real Madrid lakini hajapata kuungwa mkono na mkufunzi wa timu hiyo Zinedine Zidane. (Sky Sports)

Gareth Bale wa Real MadridHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Manchester City itamsaini mshambuliaji wa Benfica na Ureno Joao Felix, 19, iwapo itamuuza mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus 22 . (A Bola – in Portuguese)

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Bayern hawafurahii ukufunzi wa timu hiyo chini ya kocha Niko Kovac. (Bild – in German)

Winga wa Swansea Danile James 21 ananyatiwa na Newcastle huku mshambuliaji wa Uhispania Ayoze Perez, 25, akitathmini uhamisho wa dau kubwa kuelekea Itali. (Mirror)

Alexis Sanchez

Ajenti wa Alexis Sanchez ameanza mazungumzo na Inter Milan kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 raia wa Chile kuhamia katika klabu hiyo kutoka Manchester United. (Gazzetta dello Sport)

Kipa wa taifa la Czech Petr Cech, 36, alikubali kwamba kibarua chake katika klabu ya Arsenal kilikwisha miezi kadhaa iliopita. (Evening Standard)

Everton inakabiliwa na ushindani mkubwa kumfanya Andre Gomes kuondoka katika klabu ya Barcelona huku Arsenal ikijiunga na klabu ya Roma na Inter Milan katika kuisaka saini ya kiungo huyo wa kati wa Ureno, 25. (Sun)

Nahodha na beki wa klabu ya Ajax mwenye umri wa miaka 19 Matthijs de Ligt amekataa fursa ya kujiunga na Manchester United msimu huu .(Daily Mail)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents