AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi hii, Koulibaly, Kompany, Werner, Messi, Sarri

Manchester United wamewekeza nguvu zao kuwasajili wachezaji wanne mwishoni mwa msimu ambao ni: Kalidou Koulibaly, 27, kutoka Napoli, Lucas Hernandez, 22, wa Atletico Madrid, Nikola Milenkovic, 21, wa Fiorentina na Douglas Costa, 28, wa Juventus. (Mirror)

Nahodha wa Manchester City Vincent Kompany anatarajiwa kukubali kukatwa mshahara ili kusaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi na klabu hiyo. Mlinzi huyo raia wa Ubelgiji, 32, anatarajiwa kuandaliwa mchezo wa kumbukumbu mwezi Agosti mwaka huu. (Mail)

Kalidou Koulibaly, 27.

Wachezaji wa Liverpool Naby Keita na Sadio Mane wamemshawishi streka wa Ujerumani Timo Werner, 22, kuhamia Anfield iwapo ataondoka RB Leipzig mwishoni wa msimu. (ESPN)

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu ametangaza kuwa mshambuliaji raia wa Argentina Lionel Messi, 31, anatarajiwa kuongeza mkataba wake na klab hiyo. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2021. (RKB, via Marca)

Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri yupo kwenye shinikizo kubwa la kushinda taji la Europa ili kulinda kibarua chake. (Telegraph)

Juventus wamegoma kumuuza mshambuliaji wao raia wa Argentina Paulo Dybala, 25, mwishoni mwa msimu. Hilo ni Pigo kwa Manchester United na Chelsea ambao walikuwa wanamnyemelea. (Sun)

Manchester United wanatarajiwa kutangaza dau la usajili kwa winga wa Benfica Joao Felix, 19, mwishoni mwa msimu. (Sun)

Manchester City wataminyana na Manchester United katika mbio za kumsajili kiungo wa Lyon, Mfaransa Tanguy Ndombele, 22, mwishoni mwa msimu. (Sun)

Kocha wa Leicester Claude Puel amesema kupokea ofa kutoka kwa Manchester City, Manchester United na Tottenham ili kuwasajili wachezaji Ben Chilwell, Harry Maguire na James Maddison mtawalia kunaonesha namna gani klabu yake inavyofanya kazi nzuri ya kukuza vipaji. (Leicester Mercury)

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW